Katika kuelekeza nguvu kazi ya kutatua changamoto za vijana kwa njia ya uwasilishwaji wa hoja za kimantiki katika njia ya bunge, vijana kutoka Tanzania chini ya mradi wa Bunge la Vijana Afrika Mashariki siku ya leo tarehe 15th Oktoba 2021, walikutana chou kikuu Dar es salaam na wengine kwa njia ya mtandao, hususani watu wa mkoani kam Geita, Kagera, Chato, Tanga, Simiyu , bukoba nk. Kumchagua spika wao wa Mkutano na makatibu wenye dhamana ya kuendesha mkutano na kukubaliana kwa maadhimio ya uwasilishwaji wa hoja kwa ajili ya matekelezo katika Bunge la Vijana Afrika Mashariki.
Mradi Huu, ukiwa Chini ya  Taasisi ya Faraja Africa Foundation wakishirikiana na Bunge la Afrika Mashariki na taasisi zisizozakiserikali kama success hands na Tunaweza. Mheshimiwa spika mteule wa mkutano huu aliyeshinda kwa kura 94% ni Mhe.Novatus Marandu akifwatiwa na naibu spika aliyeongoza kwa kura 87% Mhe. Khayman Yakuti.
Katika Mkutano huu,Hoja tatu zilijadiliwa na kufikiwa makubaliano ya kuwasilishwa katika Bunge la Vijana Afrika Mashariki mnamo tarehe 11-12 Oktoba 2021. Hoja zilizojadiliwa ni kama zifuatazo:
- Hoja ya Azimio ya Vijana ya kuiomba serikali kuondoa sheria ya makato ya tozo za mialmala ya simu kwa kuwa si Rafiki kwa watu wakipato cha chini, vijana wa vyuo vikuu na wanaoishi vijijini.
- Hoja ya Azimio la kuiomba serikali kushughulikia changamoto za unyanyasahi wa kijinsia wa nyumbani na ukatili wa kijinsia zinazowakabili Watoto, wasichana na wanawake katika wakati wa janga hili wa UVIKO-19.
- Hoja ya kuiomba serikali kuunda benki ya maendeleo ya vijana kwa ajili ya kuwasaidia vijana ambao hawakopesheki na taasisi za kibenki na kupata mkopo wa riba nafuu.
Hoja hizi kwa ujumla wake, zilijadiliwa na mapendekezo yalitolewa katika mstakabadhi ya namna sahihi, changamoto za vijana katika ngazi hizo kuu tatu zinaweza kutatuliwa.
Pamoja na makubaliano yakimkakati yaliyojadiliwa katika siku hiyo nchini Tanzania ni Pamoja na;
- Serikali kutengeneza mazingira Rafiki katika swala zima la kurepoti matendo ya unyanyasaji wa kijinsia hususani huongezeko la mda wa kazi mpaka masaa 24 kwenye dawati la jinsia.
- Serikali kutengenza mazingira rafiki katika uombaji wa mkopo kwa vijana kutoka ngazi ya halmashauri mpaka ngazi ya kutengeneza kitengo cha benki ya maendeleo ya vijana.
- Serikali kuangalia kwa jicho la tatu swala la elimu hususani yenye kukidhi mahitaji ya karne ya 21 kwa kuimairisha teknolojia na elimu.
Kama Taasisi, Faraja Africa Foundation Pamoja na wadau wamaendeleo tunaamini katika Nguvu ya kijana kutatua changamoto zake mwenyewe kupitia Nyanja sahihi ya Uongozi uliowekwa kwa njia ya mazungumzo.
By Thekla Axel Schulte
Country Coordinator Tanzania